Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Baada ya kupita miaka 103 tangu lilipopitishwa Azimio la Balfour, swali linaloulizwa hivi sasa ni je, Uingereza, ilikuwa na nafasi gani katika vuta nikuvute ya mgogoro wa Palestina na Israel?
Uingereza ndilo dola la kwanza la Magharibi ambalo lilichangia kuasisiwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mara ya kwanza, uchangiaji na uungaji mkono huo ulichukua sura rasmi kupitia Azimio la Balfour. Azimio la Balfour lililopitishwa tarehe Pili Novemba 1917 lilifungua njia ya kuundwa utawala bandia wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa dola la kikoloni la Uingereza katika ardhi ya watu wa Palestina.
342/